KAMBI YA VIJANA YA KILIMO

Je, kilimo ni biashara yenye faida inayostahili kuwekezwa na vijana? Ndiyo, bila shaka, tunasema! Kupitia mbinu inayowajumuisha vijana, kozi hii ya wiki moja itawafunza washiriki kuhusu mazoea endelevu ya kilimo na ujuzi wa Maisha na kuonyesha jinsi kilimo kinavyoweza kuwa biashara inayovutia kwa vijana. Kozi imeundwa kuwafanya vijana wafurahie kukaa kwao katika Kituo cha Mafunzo ya Wakulima kupitia michezo na burudani huku wakati huo huo wakipata maarifa muhimu kuhusu uendelezaji wa biashara za kilimo kwa maisha bora.

Utakayo Jifunza

Kuna fursa mbalimbali za kuzalisha mapato kwa vijana. Katika kozi hii, utajifunza kuhusu…

  • Uanzishaji wa bustani za mboga katika maeneo ya vijijini na mijini
  • Uanzishaji wa vitalu vya miti
  • Ujasiriamali
  • Kuweka akiba na kukopesha katika vikundi
  • Utengenezaji wa sabuni (sabuni ya maji na ya mche)
  • Usindikaji wa chakula na uongezaji thamani
  • Ujuzi muhimu wa Maisha
  • Usimamizi wa taka
  • Michezo na burudani

Malengo ya kozi

Katika kozi yote, vijana wanawezeshwa kukuza hamu ya kilimo kama biashara kupitia uwezeshaji wa mwingiliano wa ngazi kwa ngazi na mazingira ya kujifunza yanayowafaa vijana.

Baada ya kushiriki katika kozi hizi, washiriki wanapaswa kuwa na uwezo wa…

  • Kuboresha maisha yao kwa kuendeleza na kuendesha biashara zenye faida za kilimo.
  • Kuendeleza fursa za mapato kupitia ujuzi mbalimbali wa ujasiriamali waliofunzwa, mfano, uongezaji thamani, sabuni, vitalu vya miti, na utengenezaji wa briquettes.

Kozi za 2025

11 Agosti – 15 Agosti 2025 — Namba ya Kozi: AY

8 Septemba – 12 Septemba 2025 — Namba ya Kozi: AY

Tafadhali kumbuka kuwa ratiba yetu ya mafunzo inaweza kubadilika kutokana na mahudhurio tofauti ya kozi. Ili kuthibitisha tarehe za kozi, wasiliana nasikama ilivyo onyeshwa hapa chini.

Ada ya Mafunzo: TZS 400,000 kwa kila mshiriki

(KUMBUKA: kila kitu kingine ni sawa na katika kozi ya kwanza)

Fomu ya Usajili

Jisajili sasa kwa kozi zetu za mafunzo na upate ujuzi muhimu katika kilimo endelevu! Tafadhali jaza fomu hapo chini na taarifa zako za mawasiliano, chagua kozi unayotaka kuhudhuria na tarehe unayopendelea. Chaguo la malipo linapatikana wakati wa usajili.

-
+
Malipo ya Bank au Simu - (Kama simu, tafadhali andika namba)
KAMBI YA VIJANA YA KILIMO
11th August – 15th August 2025 — Course ID: AY
8th September - 12th September 2025 — Course ID: AY
Asante kwa kujisajili kwa kozi na sisi! Maelekezo zaidi yametumwa kwa anwani yako ya barua pepe. Tafadhali angalia kasha lako la kuingia (inbox) na kasha lako la barua taka (spam). Tunatarajia kukutana nawe katika kozi zetu za mafunzo. Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia training@kilimo.org.
Oops! Something went wrong while submitting the form.