Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania (SAT)
Ni shirika lisilo la kiserikali na dira yake ni kuwa na wakulima wengi wanaoutumia mbinu za kilimo endelevu ili kuboresha maisha yao, na kuhifadhi mazingira.
Kilimo hai ni mfumo wa kilimo ambao hutumia mbinu za kuhifadhi na kukuza rutuba ya udongo, kuhifadhi viumbehai na kudhibiti visumbufu (wadudu, magonjwa na magugu) bila kutumia kemikali zinazo athiri mazingira yetu.
Ni shirika lisilo la kiserikali na dira yake ni kuwa na wakulima wengi wanaoutumia mbinu za kilimo endelevu ili kuboresha maisha yao, na kuhifadhi mazingira.
Shirika la SAT lilianzisha kituo cha kwanza cha mafunzo ya kilimo hai kwa mkulima, wajasiriamali, maafisa ugani na wafanyanyakazi nchini Tanzania kilichopo Kijiji cha Vianzi mkoani Morogoro mnamo mwaka 2013. Kituo hiki hutoa mafunzo mbalimbali zaidi ya kumi na nne (14+) kwa kutilia mkazo mafunzo kwa vitendo. Kituo kina eneo lenye ukubwa wa ekari 918,na hutoa huduma za malazi,chakula na usafiri kwa washiriki wote wa mafunzo. Mpaka sasa wakulima Zaidi ya 8000 wamepatiwa mafunzo katika kituo hiki.
Kwa kupitia jarida la MkM, SAT huwafikia wakulima wadogo na wadau wengine wa kilimo wasiopungua 180,000 kila mwezi. MkM huchapisha mada zinazoelekeza mafunzo kwa vitendo, yanayoeleweka kwa urahisi. Jarida hili limekuwa likichapishwa kwa zaidi ya miaka kumi, na ni jarida la muda mrefu zaidi na huchapisha mada mahususi za kilimo hai nchini Tanzania.
Linaaminiwa na wasomaji wake na kusaidia wakulima kufanya maamuzi sahihi ili kuzalisha chakula bora kwa ajili ya familia zao, jamii na masoko. Shirika la SAT ndio wachapishaji wa jarida hili na hutumika kama njia ya kuwapasha habari wakulima wake.
Changia kudhibiti ongezeko la hewa ukaa (CO2) kwa kupanda miti kupitia wakulima wetu. Kwa mchango wako, wakulima wadogo watawezeshwa kupanda miti kupitia kipato kidogo utakachochangia ili kutunza mazingira. Je utapanda miti mingapi?
Shirika la kilimo Endelevu Tanzania (SAT) ni mwangalizi na mshauri wa kampuni ya SAT Holistic Group Ltd ambayo ni kampuni ya kijamii inayomilikiwa na ushirika wa wakulima. Kampuni hii huwaunganisha wakulima zaidi ya 3,500 na masoko ya ndani na nje ya nchi, na huhamasisha matumizi ya mbinu endelevu za kilimo ili kupunguza umaskini.
SAT Holistic Group Ltd inamilikiwa na wakulima kwa asilimia 45%, wawekezaji wa kimkakati kwa 25% na waanzilishi (30%). Wajumbe wa bodi ni wakulima wenyewe.