Kilimo cha kudumu ni kozi inayotambulika kimataifa, inayoendeshwa kwa muda wa wiki mbili na utafanikiwa kupata Cheti cha kilimo cha Kudumu. Mafunzo haya yanatoa utangulizi wa kilimo cha kudumu ilivyofafanuliwa na mwanzilishi wake Bwana Bill Mollison.

Kozi hii ya wiki 2 huwezeshwa kwa lugha ya Kiswahili na itakujengea uwezo katika kupanga na kutumia mbinu jumuishi ili kuandaa mfumo thabiti, stahimilivu kwa mazingira ili kuendeleza maisha katika jamii na kutunza mazingira. Mkazo zaidi unawekwa katika kuboresha mazingira katika nchi za kitropiki na hasa maeneo yenye ukame. Hii itawawezesha walengwa kupanga na kuboresha mazingira kwa muundo wa asili na kwa kupangilia mifumo yenye kuleta ufanisi zaidi na inayoendeshwa kwa gharama za chini na yenye tija.
Utajifunza yafuatayo;

Malengo ya kozi

Hii kozi itafanyika ndani ya wiki mbili, kwa nadharia, mazoezi ya mbinu za kudumu na vitendo. Kozi hii itafanyika kwenye kituo chetu cha mafunzo.
Ratiba ya kozi
Hii kozi itafundishwa na wafanyakazi waSAT ambao wamefundisha zaidi ya wakulima 3000, maafisa ugani, wanafunzi wa mashuleni na vyuoni na watu wengine kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania kuhusu kilimo endelevu.
Wiki ya 1
Wiki ya 2
Kozi 2026
Tafadhali kumbuka kuwa ratiba yetu ya mafunzo inaweza kubadilika kwa sababu ya mahudhurio tofauti ya kozi. Ili kuthibitisha tarehe za kozi wasiliana nasi kama ilivyoonyeshwa hapa chini.
Ada ya Mafunzo: TZS 650,000 kwa kila mshiriki
Jisajili sasa kwa kozi zetu za mafunzo na upate ujuzi muhimu katika kilimo endelevu! Tafadhali jaza fomu hapo chini na taarifa zako za mawasiliano, chagua kozi unayotaka kuhudhuria na tarehe unayopendelea. Chaguo la malipo linapatikana wakati wa usajili.