MSINGI YA UZALISHAJI WANYAMA

Ufugaji wa mifugo na uzalishaji wa mazao unaweza kuendana vizuri sana. Vipengele vyote viwili vinaweza kutumika kwa njia jumuishi kuanzisha mzunguko fungwa wa usimamizi wa virutubisho – kanuni muhimu ya kilimo hai. Zaidi ya hayo, uuzaji wa nyama, samaki, maziwa, na asali safi unaweza kuongeza kipato cha kaya kwa wakulima wadogo kwa kiasi kikubwa. Kozi hii inatoa utangulizi kuhusu afya ya wanyama, ulaji, malazi, na uzalishaji kwa ujumla.

Ufugaji wa mifugo na uzalishaji wamazao unaweza kuendana vizuri sana. Vipengele vyote viwili vinaweza kutumikakwa njia jumuishi kuanzisha mzunguko fungwa wa usimamizi wa virutubisho – kanuni muhimu ya kilimo hai. Zaidi ya hayo, uuzaji wa nyama, samaki, maziwa, naasali safi unaweza kuongeza kipato cha kaya kwa wakulima wadogo kwa kiasikikubwa. Kozi hii inatoa utangulizi kuhusu afya ya wanyama, ulaji, malazi, nauzalishaji kwa ujumla.

Utakayo Jifunza

Ili kuendesha biashara ya mifugo kwa mafanikio, mazoea mazuri ya usimamizi yanahitajika. Mwaka huu tuna kozi mbili zenye mwelekeo maalum: Kozi ya Kwanza (AP I), yenye utangulizi wa ufugaji wa kuku, nguruwe, na samaki, na Kozi ya Pili (AP II), yenye utangulizi wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na nyuki. Kila kozi itakuwa na utangulizi wa msingi pamoja na mafunzo kuhusu…

  • Afya ya Wanyama
  • Mimea tiba kwa magonjwa mbalimbali ya wanyama na chanjo
  • Udhibiti wa kupe katika mifugo kwa kutumia tiba asilia
  • Malazi ya wanyama
  • Ulaji wa mifugo (wanyama wanaocheua na wasiocheua)
  • Kilimo cha hydroponics
  • Uandaaji wa silage

Malengo ya kozi

Baada ya kushiriki katika kozi hizi, washiriki wanapaswa kuwa na uwezo wa…

  • kuwa na wanyama wenye afya na kuwalisha ipasavyo.
  • kuongeza kipato chao cha kaya kupitia uzalishaji wa maziwa, ufugaji wa nyuki, kuku, nguruwe, na/au ufugaji wa samaki.
  • kuongeza uzalishaji wa mashamba kupitia ujumuishaji wa wanyama wa shamba na urejelezaji wa virutubisho.

Kozi za 2025

  • 14 Julai – 18 Julai 2025 — Namba ya Kozi: AP I (Utangulizi waufugaji wa kuku, nguruwe, na samaki)
  • 15 Septemba - 19 Septemba 2025 — Namba ya Kozi: AP II (Utanguliziwa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na nyuki)

Tafadhali kumbuka kuwa ratiba yetu ya mafunzo inaweza kubadilika kutokana na mahudhurio tofauti ya kozi. Ili kuthibitisha tarehe za kozi wasiliana nasi kama ilivyoonyeshwa hapa chini.

Ada ya Mafunzo: TZS 500,000 kwa kila mshiriki

(KUMBUKA: kila kitu kingine ni sawa na katika kozi ya kwanza)

Fomu ya Usajili

Jisajili sasa kwa kozi zetu za mafunzo na upate ujuzi muhimu katika kilimo endelevu! Tafadhali jaza fomu hapo chini na taarifa zako za mawasiliano, chagua kozi unayotaka kuhudhuria na tarehe unayopendelea. Chaguo la malipo linapatikana wakati wa usajili.

-
+
Malipo ya Bank au Simu - (Kama simu, tafadhali andika namba)
MSINGI YA UZALISHAJI WANYAMA
14 July – 18 July 2025 — Course ID: AP I (Introduction to poultry, piggery, and fish farming)
15 September - 19 September 2025 — Course ID: AP II (Introduction to dairy and beekeeping)
Asante kwa kujisajili kwa kozi na sisi! Maelekezo zaidi yametumwa kwa anwani yako ya barua pepe. Tafadhali angalia kasha lako la kuingia (inbox) na kasha lako la barua taka (spam). Tunatarajia kukutana nawe katika kozi zetu za mafunzo. Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia training@kilimo.org.
Oops! Something went wrong while submitting the form.